DIGITAL INCOME SYSTEM đź’ˇ
SEHEMU YA KWANZA:
"Simu Yako, Duka Lako"
✍️ Swabur|Digital Income Master
STEP 1: Tambua Mahitaji – Niche, Need, Problem & Maswali ya Watu
Lengo:
Kukusaidia kugundua tatizo halisi la watu ambalo unaweza kulitumia kama msingi wa biashara yako ya digitali kwa kutumia simu.
🔍 "Biashara yoyote inayoingiza pesa hutatua tatizo..."
Watu wanalipa ili wapate mwelekeo, wapunguze maumivu, au wapate matokeo.
Unapaswa kuanza kwa kuuliza:
- Watu wana matatizo gani?
- Wanauliza maswali gani?
- Wako wapi (WhatsApp, Telegram, TikTok, mtaani)?
- Una ujuzi, uzoefu au maarifa gani yanayoweza kuwasaidia?
Usiunde bidhaa kama ebook, kozi au huduma yoyote ya kuuza bila kuelewa kwanza shida ya soko...
Mfano...:
- Niche: Vijana wasiokuwa na ajira
- Need: Kutengeneza pesa kupitia simu
- Problem: Wanatumia simu kwa starehe, si kwa kipato
- Swali: “Nawezaje kutumia WhatsApp kutengeneza hela?”
👉 Hapa ndipo unatengeneza huduma ya kozi au mentorship ya "WhatsApp Marketing ya Kipato"
📝 Activity (Kazi ya kufanya):
- Taja matatizo 3 unayosikia watu wakilalamikia kila siku.
- Andika maswali 3 ambayo marafiki wako wamekuuliza mara kwa mara.
- Chagua moja ambalo unaweza kusaidia kulitatua leo.
5 Maoni
Maalifa ya mipangilio hii yamenifundisha kitu
JibuFutaNina imani kubwa kuhusu mitandao
JibuFutaHuko mtaani malafuki wengu hawana imani na mitandao hivyo wengi wanaona ni utapeli kwa kuwa mimi nimefatilia kwa mda mlefu naamini hiki kitu kipo na kuna watu wanalipwa kupitia sim zao
JibuFutaNi kweli kabisa
FutaVijana tuamke katika kuzitafuta fursa za kimtandao
JibuFuta